UONGOZI wa Singida Big Stars umeweka wazi kuwa mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Rayorn Sports ya Rwanda umewapa mbinu za kuikabili Dodoma Jiji pamoja na mechi nyingine za kirafiki.
Septemba 4,Singida Big Stars ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayorn Sports ya Rwanda na walitoshana nguvu bila kufungana.
Ofisa Habari wa Singida Big Stars, Hassan Masanza alisema kuwa mchezo wao dhidi ya Rayorn Sports umewapa nguvu ya kuendelea kufanya vizuri.
“Tumecheza mchezo wa kirafiki nchini Rwanda na wachezaji kuna kitu wamekipata na benchi la ufundi limeona namna hali ilivyo hivyo hiyo itatuongezea nguvu kwenye kupambana katika mechi zetu.
“Tumerejea nyumbani tunawakaribisha Dodoma Jiji tutacheza kwa kufuata kanuni ili kila mmoja aweze kufurahia soka letu,” alisema Masanza.
Jumapili watacheza na Dodoma Jiji Uwanja wa CCM Liti ikiwa ni mchezo wao wa tatu wa ligi kwa msimu wa 2022/23.
Timu hiyo inanolewa na Kocha Mkuu, Hans Pluijm imecheza mechi mbili na kushinda zote msimu wa 2022/23 ikiwa na pointi sita kibindoni.