KISINDA ATAJA SABABU ZA KUREJEA NDANI YA YANGA

TUISILA Kisinda kiungo wa Yanga ameweka wazi kuwa amereja kwa mara nyingine kufanya kazi ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Winga huyo wa Yanga amerejea kwa mara nyingine ndani ya Yanga baada ya kuuzwa msimu uliopita ndani ya kikosi cha RS Berkane ya nchini Morocco.

Amerudi kwa mara nyingine kuitumikia Yanga ambao walitwaa ubingwa msimu wa 2021/22 Kisinda aliposepa ndani ya kikosi hicho.

Nyota huyo anayeaminika kucheza mpira wa kasi ulikuwa ni usajili wa kufungia kazi kwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi akitajwa kuja kwa mkopo.

“Nimerejea tena Yanga, Yanga ni timu kubwa na kwangu ni kama familia hivyo nimekuja nina matumaini ya kufanya makubwa kwa kushirikiana na wachezaji wengine,” amesema.

Kisinda anaungana na mastaa wengine wapya ndani ya kikosi hicho ikiwa ni pamoja na Aziz KI, Bernard Morrison, Gael Bigirimana pamoja wengine waliokuwa kwenye kikosi hicho Fiston Mayele, Bakari Mwamnyeto.