MAUJUZI YA CHAMA, SAKHO KUWAONA NI BURE KABISA

BAADA ya mechi mbili za kirafiki nchini Sudan, leo Septemba 3,2022 kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Zoran Maki kitamenyana na Arta Solar saa 4:00 asubuhi, Uwanja wa Uhuru.

Mchezo wa kwanza kwenye michuano maalumu ambayo Simba walialikwa walishinda mabao 4-2 dhidi ya Asante Kotoko na ule wa pili walipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Al Hilal.

Huu ni mchezo maalumu kwa ajili ya kuendelea kujiweka sawa kwa mechi za kitaifa na kimataifa ambazo Simba itacheza msimu wa 2022/23.

Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba ameweka wazi kwamba mechi zote ambazo wanacheza wanazichukulia kwa umakini ili kupata matokeo chanya.

“Kila mchezo kwetu tunauchukulia kwa umuhimu lengo ni kupata matokeo chanya inawezekana hasa ukizingatia kwamba wachezaji wanajituma na kutimiza majukumu yao,”.

Mchezo wa leo ambao unatarajiwa kuchezwa mapema utakuwa mubashara Azam TV na  na hakuna kiingilio.

Hivyo mashabiki wa mpira leo wataona ujuzi na uwezo wa mastaa wa Simba ikiwa ni pamoja na Pape Sakho, Clatous Chama bure kabisa.