KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Honour Janza ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Uganda.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa leo Septemba 3,2022 jijini Kampala, Uganda huku akiweka wazi kwamba wapo tayari kwa mchezo wa leo.
Itakuwa ni Uwanja wa St Marys kwenye mchezo wa mkondo wa pili kumenyana na Uganda kusaka tiketi ya kushiriki Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani, (CHAN 2023).
Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Stars ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0, Jumapili iliyopita.
“Tunajua ni nini Watanzania wanataka kuona tukifanya na hasa mbele ya Uganda kutokana na kile ambacho kilitokea kwenye mchezo wa kwanza kwetu nyumbani.
“Tuna deni lakini bado tuna imani ya kufanya maajabu tukiamini kwamba lolote linawezekana,”.
Jana wachezaji wa Stars walifanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa leo kwa makipa walikuwa ni Aishi Manula, Beno Kakolanya na Aboutwalib Mshery huku kocha wao akiwa ni Tanzania One, Juma Kaseja.