SIMBA YAPOTEZA MBELE YA AL HILAL

KIKOSI cha Simba kimepoteza mchezo wake wa pili wa kirafiki kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Al Hilal.

Mchezo wa leo ni wa pili kwa Simba kucheza ikiwa nchini Sudan ambapo ilialikwa kwenye mashindano maalumu yaliyoandaliwa na Klabu ya Al Hilal.

Katika mchezo wa kwanza Simba ilishinda mabao 4-2 dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana.

Bao pekee la ushindi kwa Al Hilal limefungwa na John Mano dakika ya 62 na kuwafanya Simba kupoteza mbele ya wenyeji wao.

Nyota Gadiel Michael alikwama kuyeyusha dakika 90 baada ya kupata maumivu na nafasi yake ilichukuliwa na Okwa huku mshambuliaji mzungu wa Simba Dejan akianza kikosi cha kwanza kwenye mchezo huo.