YANGA WAJA NA MBINU TOFAUTI DHIDI YA AZAM FC

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amebainisha kuwa watabadilika kwenye mchezo wao ujao dhidi ya Azam FC utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 6,2022.

Mchezo huo unakuwa ni kwanza kwa Yanga kucheza ikiwa nyumbani baada ya kucheza mechi mbili kwenye mechi za ugenini.

Nabi amesema:”Michezo ijayo ya ligi hatutacheza sawa na ile ya ugenini kwani tutakuwa nyumbani, tunafahamu ni migumu na ngumu kusema kama tutashinda au kuingia na akili sawa na mechi iliyopita.

“Lazima tubadilike kwa kuwa tunaamini ni michezo migumu na ushindi ni jambo ambalo tunalihitaji hasa kwenye mechi ambazo tunacheza uwanjani,” amesema.

Yanga imeshinda mechi mbili za awali msimu huu wa 2022/23 ilianza mbele ya Polisi Tanzania 1-2 Yanga, Coastal Union 0-2 Yanga kwenye mechi ziliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.