SHIRIKISHO la Soka Tanzania, (TFF) limetangaza kufikia makubaliano ya kumuondoa kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Kim Poulsen kwenye benchi la ufundi pamoja na wasiaidizi wake.
Alipoteza mechi 7 alipata ushindi kwenye mechi 6 na sare kwenye mechi nne alipewa mkataba wa miaka mitatu kuinoa timu ya Stars.
Kocha huyo alichukua mikoba ya Ettiene Ndayiragije ambaye alikuwa akiinoa timu ya Stars alipewa timu hiyo 2009 Ndayiragije ambapo alijiunga na Stars akitokea Azam FC.
Kim alitangazwa kuwa Kocha Mkuu wa Stars na TFF, Februari 15,2021.
Ikumbukwe kwamba Poulsen aliwahi kuwa kocha wa Stars mwaka 2012 na 2013 kwa sasa atabaki kuwa na timu za Taifa za Vijana mpaka mkataba wake utakapokamilika.
Mchezo wa mwisho kukaa benchi akiwa na wasaidizi wake ikiwa ni pamoja na Shadrack Nsajigwa ilikuwa ni jana Julai 28 kwenye mchezo dhidi ya Uganda Stars ilipopoteza kwa kufungwa bao 1-0.
Stars kwa sasa itakuwa chini ya kocha Hanour Janza akisaidiwa na Meck Maxime na kocha wa magolikipa atakuwa ni Juma Kaseja.