LIVERPOOL WANASIFA KWELI WACHAPA 9-0

IKIWA Uwanja wa Anfield, Klabu ya Liverpool imeibuka na ushindi mkubwa wa mabao 9-0 dhidi ya Bournemouth kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

Huu unakuwa ni ushindi mkubwa ndani ya Ligi Kuu England ambayo imeanza kwa kasi na wa kwanza kwa Liverpool inayonolewa na Jurgen Klopp.

Staa Robert Firmino ambaye anafikisha mabao 100 akiwa na Liverpool  alipachika mabao mawili dakika ya 31,62 mengine ni mali ya Luis Diaz dakika ya 3,85, Harvey Elliott dakika ya 6.

Pia nyota Trent Alexander-Arnold alitupia  dakika ya 28,Virgil van Dijk beki kisiki alitupia bao moja dakika ya 45 na moja la kujifunga kwa nyota wa Bournemouth dakika ya 46 anaitwa Chris Mepham

Liverpool inafikisha pointi 5 ikiwa nafasi ya 8 kwenye msimamo huku vinara wakiwa ni Arsenal wenye pointi 12..