SIMBA QUEENS KUSAKA UBINGWA KIMATAIFA LEO

SIMBA Queens leo ina kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya She Corporate ya Uganda kwenye mchezo wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ukanda wa Cecafa.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa leo Agosti 27 Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku na ikishinda itatwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza.

Kocha Mkuu wa Simba Queens, Sebastian Nkoma ameweka wazi kuwa mchezo wa leo utakuwa na ushindani mkubwa ila wamejiandaa kupata ushindi.

“Mchezo utakuwa mgumu tunatambua na hasa ukizingatia kwamba mechi yenyewe ni dhidi ya timu kutoka Uganda haitakuwa kazi rahisi kupata ushindi.

“Malengo yetu ambayo tumejiwekea ni kupata ushindi na tumejipanga vizuri katika hilo tupo tayari wachezaji pia wapo tayari.

Charles Lukula, kocha wa She Corporates ameweka wazi kwamba anwafahamu wapinzani wake ila dakika 90 zitaamua.

“Tunawatambua Simba ni moja ya timu nzuri ila tunahitaji ubingwa na matokeo mazuri ili kusonga mbele,”.