Singida Black Stars vs Azam FC NBC Premier League kinawaka leo kwenye msako wa pointi tatu muhimu.
Wababe hawa wanakutana Aprili Mosi 2026 ikiwa ni mchezo pekee utakaochezwa mara baada ya mapumziko yaliyotokana na kalenda ya FIFA.
Katika mechi mbili kubwa wenyeji wakiwa nyumbani ndani ya mwezi Machi waliangasuha pointi tatu baada ya dakika 90.
Ilikuwa Singida Black Stars 0-3 Yanga SC na Singida Black Stars 1-2 Simba SC leo wana kazi nyingine mbele ya matajiri wa Dar, Azam FC iliyo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi na pointi 29.
Msimamo Singida Black Stars vs Azam FC
POS MP W D L PTS
3. Azam FC 15 7 8 0 29
6. Singida Black Stars 15 7 4 4 25
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.