Yanga SC yampotezea Diarra, ila Metacha alikutana nacho

UONGOZI wa Yanga SC umempotezea kiaina Djigui Diarra kutokana na kitendo chake cha utovu wa nidhamu alichofanya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.

Kipa huyo raia wa Mali alikutwa na makosa mawili katika mchezo huo jambo lililopelekea kufungiwa mechi 3 huku uongozi wa Yanga SC ukibainisha kuwa umepokea taarifa za adhabu yake na wapo makipa wengine ambao watachukua nafasi yake.

Ikumbukwe kwamba Diarra alionyesha ishara ya kidole cha kati wakati akitoka uwanjani kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar na alionekana akigombana na mwamuzi jambo ambalo limepelekea apewe adhabu ya faini na kufungiwa mechi tatu.

Diarra ameadhibiwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, (TPLB) huku uongozi wa timu hiyo ukikaa kimya kuhusu kitendo hicho alichokifanya mara baada ya mchezo.

Ikumbukwe kwamba kitendo hicho aliwahi kufanya mlinda mlango Metacha Mnata kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, Yanga SC mara baada ya mchezo.

Kutokana na kitendo hicho uongozi wa Yanga SC ulitoa taarifa rasmi kuhusu kumsamisha mara moja mchezaji huyo na kuomba radhi kwa mashabiki taarifa hiyo ilitolewa 17/06/2021.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.