Singida Black Stars yaivutia kasi Azam FC

HUSSEN Masanza, Ofisa Habari wa Singida Black Stars amesema kuwa wapo tayari kwa maandalizi ya mchezo ujao wa NBC Premier League vs Azam FC.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Airtel, Aprili Mosi 2026 kwa wababe hawa wawili kusaka pointi tatu ndani ya dakika 90.

Kwenye msimamo Azam FC baada ya kucheza mechi 15, (MP) ipo nafasi ya 3, (POS). Ushindi, (W) mechi 7, imetoa sare, (D) mechi 8. Matajiri wa Dar hawajapoteza (L) mchezo.

Singida Black Stars ipo nafasi ya 6 baada ya mechi 15. Imeshinda mechi 7 na imetoa sare mechi 7. Singida Black Stars imepoteza jumla ya mechi 4 ikikusanya pointi 25.

Masanza amesema: “Tupo tayari kuelekea kwenye mchezo wetu mkubwa dhidi ya Azam FC. Tunatambua hautakuwa mchezo mwepesi lakini tupo tayari kuhakikisha tunapata matokeo mazuri.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kwenye mchezo wetu malengo nikuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu,”.

Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye maandalizi kuelekea mchezo huo ni Khalid Aucho, Metacha Mnata.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.