NBC Premier League inaendelea ambapo Jumamosi na Jumapili kuna mechi kali mbili kwa kila timu kupambania pointi tatu muhimu.
Machi 21, 2026 ni Mtibwa Sugar vs Yanga SC, saa 10:00 jioni.
Mtibwa Sugar wapo nyumbani, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma,watakabiliana na Yanga SC.
Mchezo uliopita Mtibwa Sugar ilipoteza kwa kufungwa 3-0 dhidi ya Azam FC mchezo wa ligi, Februari 25, 2026 Uwanja wa Azam Complex.
Pia ilipoteza mchezo wa CRDB Federation ikiwa nyumbani dhidi ya Mbuni kwa kufungwa goli 1-0.
Yanga SC imetoka kucheza mchezo dhidi ya TRA United, Machi 18, 2026 na ubao ukisoma TRA United 0-0 Yanga SC.
Jumapili
Saa 1:00 usiku, Simba SC vs TRA United, Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.
Mchezo uliopita Machi 18, ubao wa Uwanja wa Kirumba ulisoma, Pamba Jiji FC 1-1 Simba SC.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.