TRA United vs Yanga SC kupigwa kesho

TRA United vs Yanga SC kupigwa kesho Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ikiwa ni ratiba ya NBC Premier League.

Yanga SC vinara wa ligi wanaingia uwanjani wakiwa wametoka kucheza mchezo mgumu dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Mkapa.

Katika mchezo huo uliochezwa Machi 15,2026 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 0-0 Yanga SC na mchezaji bora wa mchezo alikuwa Feisal Salum.

Yanga SC na Azam FC ni timu mbili pekee ambazo hazijapoteza mchezo ndani ya NBC Premier League.

Christina Mwagala, Ofisa Habari wa TRA United ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo huo na wamefanya maandalizi mazuri ili kuleta ushindani.

“Tulikuwa tumefanya maandalizi kukabiliana na Simba SC mchezo uliahirishwa sasa tunakutana na Yanga SC, tupo tayari kwa ushindani, mashabiki wajitokeze kwa wingi,”.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.