TRA United vs Yanga SC ni mchezo unaofuata kwenye ratiba huku mabingwa watetezi wakiwakosa nyota wanne kuelekea mchezo huo kutokana na kutokuwa fiti.
Taarifa rasmi kutoka Yanga SC imeeleza kuwa wachezaji hao watakuwa nje kwa mujibu wa ripoti ya madaktari na mchezo ambao wote wataukosa ni ule unaofuata dhidi ya TRA United.
Ibrahim Abdullah (Bacca) amepata jeraha la nyonga na atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha Wiki tatu
Laurindo Dilson (Depu) amepata majeraha ya nyama za paja na atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili.
Chadrack Boka amepata jeraha la enka ya mguu wa kushoto na atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili.
Edmund John amepata jeraha la Bega na atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili.