Valverde Aitikisa Man City kwa Hat-Trick Bernabéu, Real Madrid Waongoza 3-0

Kiungo wa Real Madrid, Federico Valverde, ameandika historia kwa kufunga mabao matatu (hat-trick) katika kipindi cha kwanza, akiiwezesha timu yake kuongoza mabao 3-0 dhidi ya Manchester City kwenye mchezo wa UEFA Champions League uliopigwa katika dimba la Santiago Bernabéu Stadium.

Valverde alianza kuifungia Real Madrid bao la kwanza dakika ya 20, kabla ya kuongeza la pili dakika ya 27, na kukamilisha hat-trick yake dakika ya 42, hivyo kuwafanya mabingwa hao wa Hispania kwenda mapumzikoni wakiwa na uongozi mnono wa mabao matatu.

Katika mchezo mwingine, Paris Saint-Germain wanaelekea mapumzikoni wakiwa mbele mabao 2-1 dhidi ya Chelsea.

Mabao ya PSG yalifungwa na Bradley Barcola dakika ya 10 na Ousmane Dembélé dakika ya 40, huku bao la Chelsea likifungwa na Malo Gusto dakika ya 28.

Wakati huohuo, timu ya kushangaza kutoka Norway, FK Bodø/Glimt, inaendelea kuonyesha makali yake katika mashindano hayo baada ya kuongoza mabao 2-0 dhidi ya vigogo wa Ureno, Sporting CP.

Matokeo ya muda wa mapumziko (HT):

  • Real Madrid 3-0 Manchester City
    ⚽ 20’ Valverde
    ⚽ 27’ Valverde
    ⚽ 42’ Valverde

  • PSG 2-1 Chelsea
    ⚽ 10’ Barcola
    ⚽ 28’ Gusto
    ⚽ 40’ Dembélé

  • Bodø/Glimt 2-0 Sporting CP