CAF Yatangaza Waamuzi wa Afrika kwa Kombe la Dunia la FIFA 2026

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF), limetoa orodha ya Waamuzi wa Afrika na Maafisa wa VAR waliochaguliwa kuchezesha Kombe la Dunia la FIFA 2026, huku maafisa kadhaa wenye uzoefu wakipata fursa ya kuwakilisha bara kwenye Mashindano makubwa zaidi ya Kandanda.

Michuano hiyo ya Kombe la Dunia ambayo itaandaliwa kwa pamoja kati ya Marekani, Mexico na Canada, itashirikisha wasimamizi wa mechi kutoka Afrika waliochaguliwa kulingana na uchezeshaji wao katika Mashindano mbali mbali ya Kimataifa.

Miongoni mwa Waamuzi waliotajwa ni Mwamuzi wa Mauritania Dahane Beida, ambaye kuimarika kwake katika uchezaji wa kimataifa kumeendelea kutambulika.

Orodha ya waamuzi hao pia ina waamuzi kadhaa wanaojulikana Afrika akiwemo Mustapha Ghorbal wa Algeria, Jean-Jacques Ndala Ngambo wa DR Congo, Amin Omar wa Misri na Mwamuzi wa Gabon Pierre Ghislain Atcho.

CAF pia imethibitisha Waamuzi wasaidizi wa VAR watakaoshiriki michuano hiyo.