Takribani nusu siku tokea Kamati ya Saa 72 itangaze adhabu kadhaa kwa wakosefu ambao hakika wanapaswa kujirekebisha. Lakini wazi kuonaonekana ndani yake kuna SIASA na haiwezi kuwa msaada kwa wachezaji wetu, klabu au mpira wa Tanzania.
Adhabu ya Mwalimu wa Simba ni sahihi kabisa na anapaswa kujifunza kwa kuwa alifanya shambulizi hata kama aliyeshambuliwa alianza.
Adhabu kadhaa kama za Abdi Banda na mwamuzi aliyekataa bao la Simba. Lakini Abdullah Bacca kamshambulia mchezaji wa timu pinzani kwa kumwida akimtishia kumpigia! HAKUNA ADHABU WALA ONYO!
Kweli wanakamati hawakuliona hili? Au wanafanya maamuzi kwa ushabiki au SIASA ZA SOKA?
Mchezaji kupeleka mkono kwa mchezaji mwingine kwa lengo au muonekano wa shambulizi ni kosa. Lazima kulinda taswira ya Ligi yetu ambayo imepiga hatua.
Kamati zinateuliwa ili kuisaidia TFF na Bodi ya Ligi kuendeleza mpira na si kufurahisha wanakamati au WATU FULANI…
Lazima kuwafunza na kuwakumbusha wachezaji wetu kwa nia njema ya mpira wetu na si kuwajengea mazingira ya untachable tukaona tunajenga.
Kamati inapaswa kujitathmini kama kweli ipo kwa ajili ya maendeleo ya mchezo wa soka na hakuna haja ya kuwa na hofu kuwa hawa wakimkosa huyu na yule kaumia ni shida….muhimu haki itendeke kwa faida ya mpira wa tanzania.