Simba SC 2-0 B19 FC katika mchezo wa hatua ya 32 CRDB Federation Cup, Uwanja wa Mej. General Isamuhyo.
Watupiaji ni Inno Loemba dakika ya 22 kwa pigo la kichwa na Clatous Chama dakika ya 77 akitumia pasi ya Ellie Mpanzu.
Mpanzu na Chama wote walianzia benchi mchezo wa leo. Chama alichukua nafasi ya kiungo Morice Abraham ambaye alianza kikosi cha kwanza.
Matokeo haya yanaifanya Simba SC kutinga hatua ya 16 CRDB Federation Cup ambapo mabingwa watetezi ni Yanga SC.
Mabingwa Yanga SC vs Polisi Tanzania wanatarajiwa kukutana kesho Machi 8 2026 Uwanja wa KMC Complex kusaka mshindi.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.