Yanga SC vs Simba SC taarifa mpya kuhusu Pacome

Yanga SC vs Simba SC taarifa mpya kuhusu Pacome imetolewa ambapo wababe hao wawili wanatarajia kukutana Uwanja wa New Amaan Complex.

Pacome hakuwa sehemu ya mchezo dhidi ya JKT Tanzania ambapo Yanga SC ilipata ushindi wa magoli 5-0 anatajwa kuwa huenda leo Machi Mosi akawa sehemu ya kikosi mara baada yakufanya mazoezi na wachezaji wenzake.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa New Amaan Complex saa 2:15 usiku kwa kwa saa za Afrika Mashariki wakisaka pointi tatu muhimu.

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Pedro Goncalves amesema: “Kuhusu mchezaji Pacome, ni kweli kwamba ana majeraha. Sote tulishuhudia alipoyapata katika mchezo wetu dhidi ya JS Kabylie. Kwa sasa tunaendelea kufuatilia kwa karibu hali yake kiafya na baada ya mazoezi ya mwisho tutajiridhisha iwapo atakuwa tayari na sehemu ya kikosi kwa ajili ya mchezo wetu,”.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.