SAA chache zikiwa zimebaki kabla ya mchezo wa Kariakoo Dabi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa New Amaan Complex saa 2:15 uongozi wa Simba SC umeripoti taarifa kuhusu uwepo wa matobo chumba cha kubadilishia nguo.
Yanga SC vs Simba SC zinatarajiwa kukutana leo ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa kwanza NBC Premier League.
Taarifa iliyotolewa na Simba SC kupitia ukurasa rasmi wa Instagram imeandikwa namna hii: “Kamishna wa Mchezo wa Kariakoo Derby akiwa na wasimamizi wa Uwanja wa Amaan pamoja na baadhi ya viongozi wa klabu wakikagua chumba cha kubadilishia nguo kwa wachezaji kikiwa na matobo katika maeneo mbalimbali ambayo jana katika ukaguzi wa mwisho wa uwanja hayakuwepo,”.