Simba SC wana msongo wa mawazo kisa kichapo

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kwa sasa kikosi hicho kinakabiliwa na presha kubwa na msongo wa mawazo.

Sababu kubwa inayofanya hayo yote ni kufuatia mzigo wa matokeo mabaya katika mechi 6 zilizopita za Kariakoo Dabi.

Kwenye mechi hizo Simba SC ilipoteza na kipigo kikubwa Novemba 5,2023 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga SC 5-1 Simba SC.

Leo Machi Mosi 2026, watani hawa wa jadi wanatarajiwa kukutana Uwanja wa New Amaan Comple, saa 2:15 katika msako wa pointi 3 muhimu.

Ahmed amesema:”Tunatambua umuhimu wa mchezo wetu wa Kariakoo Dabi. Kwa sasa tunakabiliwa na presha kubwa na msongo wa mawazo hii inatokana na matokeo mabaya kwenye mechi zetu zilizopita.

“Licha ya matokeo hayo bado tupo imara kwa kuwa hii ni mechi mpya hivyo tutaingia uwanjani tukiwa na ari mpya kwa lengo la kutafuta matokeo mazuri,”.

Kwenye msimamo Simba SC ipo nafasi ya 3 ikiwa na pointi 23 inakutana na Yanga SC vinara wakiwa na pointi 28 wote wamecheza mechi 10 za NBC Premier League.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.