Yanga SC vs Simba SC ni Machi Mosi 2026 kwa watani hawa kukutana Uwanja wa New Amaan Complex kusaka pointi tatu.
Tayari mwamuzi wa mchezo wa kati jina lake lipo wazi ambaye ni Nassoro Mwinchui kutoka Tanga atahukumu mchezo huo.
Yanga SC ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 28 baada ya mechi 10 wanakutana na Simba SC iliyo nafasi ya 3 na pointi 23 baada yakucheza mechi 10.
Huu unakuwa mchezo wa kwanza msimu wa 2025/26 wababe hawa kukutana uwanjani kusaka ushindi.
Simba SC mchezo wake uliopita kwenye ligi ilipata pointi moja mbele ya Dodoma Jiji FC huku Yanga SC wenyeji wakipata ushindi wa mabao 5-0 JKT Tanzania.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.