Meridianbet Yajitoa Kwa Wenye Uhitaji Mwezi Huu Mtukufu Wa Ramadhani

Wakati mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ukiwa unaendelea, Meridianbet imeonyesha mshikamano wake wa kijamii kwa kutoa msaada wa vyakula na mahitaji muhimu kwa familia zenye uhitaji wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Hatua hii imelenga kuwasaidia wananchi wanaokabili changamoto za maisha, hasa wakati wengi wakiendelea na ibada ya kufunga kila siku.

Kupitia mpango wake wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), Meridianbet imewekeza katika ustawi wa familia kwa kuhakikisha mahitaji muhimu ya nyumbani na vyakula vinapatikana kwa wale wenye uhitaji zaidi. Msaada huu unalenga kutoa nafuu na faraja kwa kaya zinazokabiliwa na hali ngumu ya maisha, hasa wakati huu muhimu wa kidini ambapo familia zinahitaji msaada wa haraka wa chakula cha kifa na mahitaji ya kila siku.

Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi! Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.

Akizungumza wakati wa zoezi la usambazaji, Nancy Ingram, msemaji wa Meridianbet, alisema: “Tunajivunia kushirikiana na jamii yetu wakati huu wa Ramadhani. Tunafahamu kuwa mwezi huu ni wa ibada, mshikamano na kutoa, na tunataka kuhakikisha kuwa familia zote zinaweza kutekeleza ibada hii kwa amani na furaha, bila shinikizo la upungufu wa chakula.”

Wanufaika walieleza furaha yao na kutoa shukrani zao, wakitambua kuwa msaada huo umefika kwa wakati muafaka. Meridianbet imetangaza kuwa huu ni mwanzo wa mradi mkubwa wa kijamii unaoendelea, ikiwemo afya, elimu, mazingira, na msaada kwa makundi yenye mahitaji maalum, kwa lengo la kujenga jamii yenye ustawi, mshikamano, na matumaini endelevu, hasa katika mwezi wa baraka za Ramadhani.