Man United Kumuuza Bruno Fernandes kwa pauni milioni 87?

Kiungo na nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes anaripotiwa kuwa kwenye rada ya vilabu vikubwa barani Ulaya pamoja na Mashariki ya Kati.

klabu ya Paris Saint-Germain, FC Bayern Munich, pamoja na vilabu kadhaa vya Saudi Arabia vinaonesha nia kubwa ya kumsajili nyota huyo raia wa Ureno.

Ripoti hiyo inaongeza kuwa Manchester United huenda ikafikiria kumuuza iwapo ofa ya takriban pauni milioni 87 (£87m) itawasilishwa hatua ambayo ingeweza kusaidia mipango ya kujenga upya safu ya kiungo.

Mpaka sasa hakuna tamko rasmi lililotolewa na Manchester United kuhusu mustakabali wa nahodha huyo na mazungumzo yakitarajiwa kushika kasi kadri dirisha la usajili linavyokaribia.