Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Gachi (Fatma Omary) ameibuka na madai mazito akimtuhumu rafiki yake wa karibu, Yammi, kwa kuhusika katika kuvunjika kwa mahusiano yake.
Akizungumza kwa hisia, Gachi amesema alimtambua Yammi kwa mpenzi wake kwa nia njema, lakini baadaye mambo yakabadilika na kusababisha kuvunjika kwa uhusiano wake.
“Nilimtambulisha Yammi kwa mpenzi wangu lakini ndiye aliyechangia kwa kiasi kikubwa kuvunjika kwa huba langu na mwanaume wangu. Bila shaka alitumia nguvu za asili maana sielewi hadi sasa jinsi alivyofanikisha mpango wake wa kuniibia mwanaume,” amesema Gachi.
Kauli hiyo imeibua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wa muziki, hasa kuhusu urafiki na mipaka katika mahusiano.
Hata hivyo, hadi sasa Yammi hajatoa tamko rasmi kujibu tuhuma hizo.
