Tottenham Yamteua Igor Tudor Kuwa Kocha Mkuu Mpya

Klabu ya Tottenham Hotspur imethibitisha kumteua Igor Tudor kuwa kocha mkuu mpya klabuni hapo kwa mkataba mpaka Juni 2026 akichukua mikoba ya Thomas Frank aliyetupiwa virago siku ya Jumatano.

Nyota huyo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Croatia amekuwa hana kibarua tangu Oktoba 2025 baada ya kutimuliwa na Juventus alikohudumu kwa miezi Saba.

Tudor 47, raia wa Croatia amewahi pia kuvinoa vilabu vya Hajduk Split, Galatasaray, Udinese, Marseille na Lazio.