Jeremy Jacquet Ajiunga na Majogoo – Liverpool Yasubiri Kibali Kutoka FIFA

Liverpool wametangaza rasmi kukamilisha usajili wa mchezaji Jeremy Jacquet, na hatua inayosubiriwa sasa ni kupatikana kwa kibali cha Kimataifa ili nyota huyo aanze kazi rasmi Anfield.

Jeremy Jacquet ni Nyota wa Ufaransa, anacheza kama Mlinzi wa kati (central defender) akitokea katika klabu ya Stade Rennais FC nchini Ufaransa na kujiunga na Majogoo hao wa Anfield.