Esperance Tunis 1-0 Simba SC CAF Champions League

Esperance Tunis 1-0 Simba SC ni matokeo kwenye mchezo wa tatu hatua ya makundi msimu wa 2025/26 kwenye msako wa pointi tatu kusaka tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali.

Goal la ushindi lilifungwa na Jack Diarra dakika ya 21 kipindi cha kwanza lilidumu mpaka mwisho wa mchezo kwa wenyeji kuvuna pointi tatu wakiwa nyumbani.

Simba SC chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker iliruhusu goli la mapema kwenye mchezo huo ikiwa ni mchezo wa tatu mfululizo inapoteza hatua ya makundi.

Nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali kwa Simba SC inazidi kuwa finyu kutokana na mwendo ambao wameanza nao ndani ya mechi za ushindani.

Mchezaji Clatous Chama ambaye ni ingizo jipya akitokea kikosi cha kwanza alianzia benchi huku Nickson Kibabage yeye alianza kikosi cha kwanza hawa wote walikuwa Singida Black Stars.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.