Nai Azungumzia Tetesi Zake na Pacome Zouzoua Kupitia Global TV

Baada ya tetesi kusambaa kwa muda mrefu mitandaoni zikimhusisha mwanadada @officiall_nai na staa wa Yanga SC, Pacome Zouzoua, hatimaye mwenyewe ameamua kuvunja ukimya.

Kupitia mahojiano ya mubashara na Global TV, Nai amefunguka na kuweka wazi ukweli kuhusu madai yanayoendelea kuzunguka mitandaoni, akieleza msimamo wake juu ya tetesi hizo zinazomhusisha na kiungo huyo wa Yanga.

Mahojiano hayo yalifanyika chini ya uendeshaji wa @gabbymtanzania80, ambapo maswali ya moja kwa moja yaliwekwa mezani na majibu yake yamezua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wa burudani na soka.

Je, tetesi hizo zina ukweli au ni porojo za mitandao?