Nje ya uwanja, Refa raia wa Ghana, Daniel Nii Laryea, amepoteza akaunti yake ya Instagram baada ya kuripotiwa kwa wingi na mashabiki wa Nigeria.
Hatua hiyo imekuja muda mfupi baada ya kumalizika kwa mechi ya Nusu Fainali ya AFCON 2025 kati ya Nigeria na Morocco, ambapo Nigeria walipoteza na kuondolewa kwenye mashindano.
Mashabiki wengi wa Nigeria wameonesha hasira zao wakilalamikia maamuzi ya refa huyo, wakidai kuwa katika mchezo huo alionesha upendeleo kwa timu ya Morocco. Malalamiko hayo yalisambaa kwa kasi mitandaoni na kusababisha akaunti yake ya Instagram kufungwa.