
Kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga SC, Allan Okello, rasmi ameanza mazoezi baada ya kujiunga na klabu hiyo akitokea klabu ya Vipers SC ambapo alikuwa miongoni mwa wachezaji tegemeo na waliokuwa wakionesha kiwango kizuri katika Ligi Kuu ya Uganda pamoja na mashindano ya kimataifa..
Okello ameonekana akifanya mazoezi ya Gym ikiwa ni sehemu ya kurejesha na kuimarisha utimamu wa mwili kabla ya kuanza mazoezi ya uwanjani.
Usajili wa kiungo huyo umepokewa kwa matumaini makubwa ndani ya klabu ya Yanga, ambayo ni moja ya klabu zenye historia kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
