WABABE wawili wanatarajiwa kukutana uwanjani kwenye msako wa bingwa mpya wa NMB Mapinduzi Cup, Januari 13,2026.
Ni Azam FC vs Yanga SC hawa watakuwa na kazi kufika hitimisho la mashindano haya ambayo yalikuwa na ushindani mkubwa katika hatua za makundi, nusu fainali na sasa fainali.
Yanga SC iliwaondoa Singida Black Stars na Azam FC iliwaonoda Simba SC kwenye hatua ya nusu fainali na timu zote zilipata ushindi wa goli 1-0 katika hatua hiyo.
Timu zote zimeanza maandalizi tayari kwa mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya uwanja ambao utatoa maamuzi nani atakuwa bingwa.
Goli la Azam FC dhidi ya Simba SC lilifungwa na Lameck Lawi ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora na lile la Yanga SC vs SBS lilifungwa na Maxi Nzengeli.
Ni mbinu za Florent Ibenge Kocha Mkuu wa Azam FC vs mbinu za Pedro Goncalves, Kocha Mkuu wa Yanga SC zitakuwa kazini msako wa taji.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.