Azam FC vs Simba SC NMB Mapinduzi Cup mchezo mkali unatarajiwa kuchezwa kesho Januari 8,2026 Uwanja wa New Amaan Complex.
Wababe hawa kutoka bara kila mmoja anaingia uwanjani akitoka kupata ushindi kwa bao la jioni mbele ya mpinzani hatua ya makundi.
Simba SC ilipambana mbele ya Fufuni FC dakika ya 90 bao la ushindi lilifungwa na Naby Camara ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora.
Azam FC mchezo wa makundi dhidi ya URA bao la ushindi lilifungwa na Alobogast dakika ya 90 ya mchezo hivyo timu zote zina uwezo wa kuamua matokeo mpaka mwisho wa mchezo.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo na wachezaji watapambana kupata matokeo mazuri.
Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC amesema wanatambua uimara wa wachezaji walionao na benchi la ufundi hivyo wanaamini watapata matokeo mazuri.
Mshindi wa mchezo wa nusu fainali ya kwanza atakutana na mshindi wa nusu fainali ya pili Singida Black Stars vs Yanga SC, Januari 9,2026.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.