Arsenal Yaendelea Kukimbia EPL Yaichapa Bournemouth 3–2 Ugenini

Arsenal imeendelea kuonesha ubabe kwenye Ligi Kuu England baada ya kupata ushindi wa tano mfululizo, mara hii wakiichapa AFC Bournemouth mabao 3–2 katika dimba la Vitality Stadium.

Licha ya wenyeji kuanza kwa kasi kupitia bao la Evanilson dakika ya 11, Arsenal walijibu haraka kupitia Magallanes dakika ya 16 na kufanya matokeo kuwa 1–1 hadi mapumziko.

Kipindi cha pili kilishuhudia Washika Mitutu wakiongeza kasi, ambapo Declan Rice alifunga bao la pili dakika ya 54 kabla ya kuongeza lingine dakika ya 71. Bournemouth walipata bao lao la pili kupitia Kroupi dakika ya 77, lakini halikutosha kuzuia Arsenal kuondoka na pointi tatu.

Kwa ushindi huo, Arsenal wamefikisha pointi 48 baada ya mechi 20, na kuendelea kuongoza msimamo wa ligi wakiwa pointi 7 mbele ya Manchester City waliopo nafasi ya tatu na mchezo mmoja mkononi.

Matokeo ya Mwisho:
Bournemouth 2–3 Arsenal