Arsenal Yapata Nafuu — Man City Yakwama Tena

Manchester City imelazimishwa sare tasa dhidi ya Sunderland kwenye Uwanja wa Stadium of Light, katika mchezo uliokuwa mkali lakini bila mabao.
Ni siku ambayo karibu michezo yote ya Ligi Kuu England imeishia bila mshindi.

Sare hiyo inaiacha Man City ikiwa alama nne nyuma ya viongozi Arsenal, ambao sasa wana pointi 41 baada ya michezo 19.
Sunderland wao wanasalia nafasi ya 7 wakiwa na pointi 29 kupitia michezo 19.

Matokeo ya Leo – EPL

  • Sunderland 0–0 Man City

  • Brentford 0–0 Tottenham

  • Liverpool 0–0 Leeds United

  • Crystal Palace 1–1 Fulham