Taifa Stars Yaweka Rekodi, Yakutana na Morocco 16 Bora AFCON 2025

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imepangwa kuvaana na Morocco katika hatua ya 16 bora ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), mchezo unaotarajiwa kupigwa Januari 4, 2026.

Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kufuzu hatua ya mtoano wa 16 bora tangu iliposhiriki kwa mara ya kwanza AFCON mwaka 1980 — hatua inayotazamwa kama mafanikio makubwa kwa soka la nchi.

Taifa Stars imefuzu kupitia nafasi ya best loser baada ya kulazimisha sare ya bao 1–1 dhidi ya Tunisia, matokeo yaliyoipa nafasi ya kusonga mbele licha ya ushindani mkali wa makundi.

Kwa upande mwingine, jirani zao Uganda wameaga mashindano hayo baada ya kukubali kichapo cha mabao 3–1 kutoka kwa Nigeria, na hivyo kukosa nafasi ya kuendelea mbele.

Mashabiki wa soka nchini wanatarajia kuona Taifa Stars ikipambana kuhakikisha inavuka hatua hii muhimu dhidi ya wenyeji Morocco.