FT: Simba SC 2-0 Yanga SC

Desemba 21,2025 kulikuwa na mchezo wa kirafiki wa Kariakoo Dabi Fans uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex, Dar.

Baada ya dakika 90 ubao umesoma Simba SC Fans 2-0 Yanga SC Fans, magoli yote yakifungwa kipindi cha kwanza.

Magoli ya Simba SC yamefungwa na Thobias Sébastien na Dr Mo haya yalidumu mpaka mwisho wa mchezo uliohudhiriwa na mashabiki wengi.

Kipa mamba moja wa Yanga SC Fans, Kobis wa Kobis ama Jobless wa Taifa mapema aliomba sub kabla ya mchezo kushika kasi.

Ni Ahmed Ally na Aly Kamwe Mameneja Idara ya Habari na Mawasiliano waliongoza jahazi la mashabiki kwenye mchezo wa leo huku Ahmed akivaa kitambaa cha unahodha kwa Simba SC Fans.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.