Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), limezindua muundo wa zawadi kwa ajili ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya AFCON 2025, yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni nchini Morocco.
Kulingana na uchanganuzi Bingwa atapata Dola za Kimarekani Milioni 7 (Shilingi Bilioni 17.3 za Tanzania) huku Mshindi wa pili akipata Dola Milioni 4 (Shilingi Bilioni 9.96 za Tanzania).
Waliofuzu nusu fainali ni Dola Milioni 2.5 kila mmoja, waliofuzu robo fainali Dola Milioni 1.3 kila mmoja.
Katika Mashindano hayo ambayo yatazishirikisha nchi 24, timu zilizoishia raundi ya 16 zitapewa Dola 800,000 ( Shilingi Bilioni 1.98 za Tanzania).
Tanzania chini ya Kocha Miguel Gamondi itaanza karata yake ya kwanza dhidi ya miamba wa soka barani Afrika Nigeria Desemba 23 majira ya saa mbili na nusu za usiku.