Wakati wengi wakijiandaa kusherehekea Sikukuu ya Krismasi, Meridianbet imeamua kuifanya sikukuu hiyo kuwa na maana zaidi kwa familia zinazopitia hali ngumu ya kiuchumi. Kampuni hiyo inayoongoza katika sekta ya michezo ya kubashiri nchini Tanzania imefika katika kata mbalimbali za Manispaa ya Kinondoni, ikitoa msaada wa mahitaji ya msingi ya nyumbani kwa familia zenye kipato cha chini, ili kuhakikisha sikukuu inawafikia wote kwa furaha.
Mpango huo umetokana na dira ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) ya Meridianbet, inayotambua kuwa msaada mdogo unaweza kuleta mabadiliko makubwa katika maisha ya watu. Vitu vilivyogawiwa vilijumuisha vyakula na vifaa muhimu vya matumizi ya kila siku kama mchele, mafuta ya kupikia, sukari, sabuni na vifaa vya usafi, vilivyoandaliwa mahsusi kusaidia kaya kukabiliana na mahitaji ya msingi katika kipindi hiki cha sikukuu.
Akielezea lengo la zoezi hilo, mwakilishi wa Meridianbet, Nancy Ingram, alisema kuwa kampuni inaamini katika kugusa maisha ya jamii kwa vitendo. “Tunaelewa hali halisi ya maisha ya wananchi, hasa wakati huu wa mwisho wa mwaka ambapo mahitaji huongezeka. Kupitia msaada huu, tunalenga kuleta faraja na kuimarisha mshikamano wa kijamii,” alisema wakati wa ugawaji wa vitu hivyo.
Meridianbet inaendelea kuwa kitovu cha burudani. Michezo ya kasino yenye ubora, mechi zenye odds zinazovutia, pamoja na urahisi wa kujiunga kupitia meridianbet.co.tz au *149*10# Ukiwa na Meridianbet, kila siku ni ukurasa mpya wa hadithi ya ushindi.
Kwa upande wao, wanufaika wa msaada huo walionesha furaha na shukrani, wakisema kuwa msaada huo umefika kwa wakati muafaka. Wengi walibainisha kuwa msaada huo umepunguza mzigo wa maisha na kuwapa fursa ya kuipokea Krismasi kwa amani, licha ya changamoto za kiuchumi zinazowakabili.
Kwa kuendeleza juhudi hizi, Meridianbet inaonesha kuwa dhamira yake kwa jamii ni ya kudumu. Mbali na msaada wa mahitaji ya msingi, kampuni imekuwa ikijihusisha na miradi mbalimbali ya kijamii ikiwemo kusaidia watoto yatima, kuchangia sekta ya afya, kuhamasisha elimu kwa vijana, kuhifadhi mazingira pamoja na kuunga mkono michezo na burudani, hatua zinazolenga kujenga jamii imara na yenye matumaini.