Kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii na mfanyabiashara Aziz K amemtumia mke wake, Hamisa Mobetto, ujumbe maalum wa pongezi katika siku yake ya kuzaliwa.
Hamisa Mobetto amefikisha umri wa miaka 30 leo, Desemba 10, 2025, na kwa mnasaba huo, Aziz K ameandika ujumbe mrefu uliojaa shukrani, upendo na pongezi kwa mwanadada huyo.
Katika ujumbe wake, Aziz K alimtakia Hamisa kheri, mafanikio na mwaka wenye baraka, huku akimsifia kwa nafasi kubwa aliyonayo katika maisha yake. Alieleza kuwa Hamisa amekuwa nguvu na msukumo wake, akimfanya kuwa mwanaume bora zaidi na mtu mwenye shukrani kubwa.
Sehemu ya ujumbe wake ilisomeka:
“On this special day, I want to remind you how much you mean to me… You are my strength, my softness, my peace, and my inspiration. Because of you, I’m a better man… Happy birthday, my queen.”
Ujumbe huo umezua hisia na pongezi nyingi kwenye mitandao ya kijamii, huku mashabiki na watu wa karibu wakimtakia Hamisa siku njema ya kuzaliwa na mafanikio zaidi katika maisha na kazi zake.
Hamisa Mobetto anaendelea kuwa mmoja wa majina makubwa katika tasnia ya mitindo, muziki na urembo, ambapo pia hivi karibuni ameonekana kushamiri katika miradi ya biashara na ubunifu.