Coastal Union 0-1 Yanga SC, NBC Premier League

Coastal Union 0-1 Yanga SC, NBC Premier League ikiwa ni mchezo wa msimu wa 2025/26 uliokuwa na ushindani mkubwa uwanjani.

Zilishuhudiwa dakika45 milango ikiwa ni migumu kwa timu zote mbili katika msako wa pointi tatu muhimu uwanjani.

Ni Prince Dube mshambuliaji namba moja wa Yanga SC alifunga bao la ushindi katika dakika za lala salama likidumu mpaka mwisho wa kipyenga.

Ilikuwa dakika ya 88 Dube ambaye alitoka kufunga katika mchezo uliopita dhidi ya Fountain Gate alifunga tena kwenyemchezo wa leo Desemba 7,2025.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.