Rais wa Marekani, Donald Trump ametunukiwa tuzo mpya ya amani ya FIFA kwenye hafla ya Droo ya Hatua ya Makundi ya Kombe la Dunia 2026 FIFA inayofanyika leo Ijumaa, Desemba 5, 2025 huko Kennedy Center Jijini Washington, D.C Marekani.
Kwa mujibu wa FIFA, tuzo hiyo inayoitwa “FIFA Peace Prize Football Unites the World” inalenga kuwatambua watu ambao wamefanya matendo ya kipekee ya kuleta amani na wamewaleta watu pamoja kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Mpaka sasa, mchakato wa uteuzi wa washindi na vigezo vilivyotumika hawajawekwa wazi, jambo ambalo limeibua maswali kutoka kwa wadadisi wa masuala ya haki na uwazi.