Mchambuzi mahiri wa soka nchini, Saleh Jembe (@salehjembefacts), ametolea ufafanuzi tetesi zinazozagaa mitandaoni kuhusu kampuni ya DP World kudaiwa kuwa katika mazungumzo ya kuidhamini Klabu ya Simba SC.
Amesema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote, na zimeibuliwa bila ushahidi wa aina yoyote kutoka kwa pande husika. Saleh Jembe ameongeza kuwa hadi sasa hakuna chanzo rasmi kutoka Simba SC wala DP World kilichothibitisha uwepo wa mazungumzo ya udhamini.
Amesisitiza kuwa mashabiki wa Simba wanapaswa kutambua kuwa taarifa za udhamini ni mambo ya kitaasisi yanayopaswa kuthibitishwa na uongozi wa klabu au kampuni yenyewe, na siyo kusambazwa kupitia vyanzo visivyo rasmi.
Hata hivyo, ameeleza kuwa ni kawaida kwa klabu kubwa kuhusishwa na kampuni mbalimbali, lakini ni muhimu kutegemea taarifa sahihi kutoka katika vyanzo vya kuaminika.