Fulham Yatoa Upinzani Mkali, Lakini Man City Yapenya 5–4

Mvua ya mabao imeshuka katika dimba la Craven Cottage, Manchester City ikiibuka na ushindi mwembamba wa 5–4 dhidi ya Fulham katika mchezo uliokuwa na msisimko mkubwa wa Ligi Kuu England.

Ushindi huo unaifanya Man City kufikisha alama 28 baada ya mechi 14, ikisalia nafasi ya pili kwenye msimamo. Fulham, licha ya upinzani mkali, inasalia nafasi ya 15 ikiwa na alama 17 baada ya idadi sawa ya michezo.

Matokeo ya Mwisho: Fulham 4–5 Man City

Magoli ya Fulham:
⚽ 45+2’ – Emile Smith Rowe
⚽ 57’ – Alex Iwobi
⚽ 72’ – Samuel Chukwueze
⚽ 78’ – Samuel Chukwueze (la pili)

Magoli ya Man City:
⚽ 17’ – Erling Haaland
⚽ 37’ – Tijjani Reijnders
⚽ 44’ – Phil Foden
⚽ 48’ – Phil Foden (la pili)
⚽ 54’ – Sander Berge (og)

Mchezo huo uligeuka sinema ya kutazamika, Man City ikitawala kipindi cha kwanza kabla ya Fulham kurudi kwa nguvu na kuzua sintofahamu hadi dakika za mwisho.

Matokeo Mengine EPL

FT: Bournemouth 0–1 Everton
⚽ 78’ – Jack Grealish

Everton yaibuka na ushindi muhimu ugenini kupitia bao la Jack Grealish dakika ya 78.