WAWAKILISHI wa Tanzania katika anga la kimataifa Simba SC baada ya kupoteza mchezo wa pili hatua ya makundi wanatarajia kuwasili kwenye ardhi ya nyumbani Novemba 2,2025.
Tayari kikosi hicho chini ya Meneja Mkuu, Dimitar Pantev kimeanza safari kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bamako Senou, Mali tayari kuanza safari ya kurejea Dar, kupitia Addis Ababa, Ethiopia.
Msafara huo wa Simba unatarajiwa kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar saa kumi kamili afajiri ya kesho Jumanne kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu Bara.
Simba imetoka kucheza dhidi ya Stade Malien katika mchezo wa pili wa hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambao ulipigwa jana Jumapili na kumalizika kwa kufungwa mabao 2-1.
Mchezo wa kwanza kwa timu hiyo ambayo nafasi yake kutinga hatua ya robo fainali inazidi kuwa ngumu imecheza mechi mbili, ikipoteza zote msimu wa 2025/26.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.