Stade Malien 2-1 Simba SC CAF Champions League

CAF Champions League matokeo ni Stade Malien 2-1 Simba SC ikiwa ni mchezo wa hatua ya makundi msimu wa 2025/26.

Taddeo Nkeng alipachika bao ka kuongoza dakika ya 16 na kamba ya pili ilifungwa na Ismail Simpara dakika ya 23 yakitosha kubakisha pointi tatu mazima kwa wenyeji.

Neo Maema alifunga bao pekee la Simba SC dakika ya 53. Mchezo wa pili Simba Sac inapoteza katika anga la kimataifa licha ya kutengeneza nafasi zaidi ya tatu ni bao moja wamepata.

Kiungo Kante wa Simba SC alikwama kukamilisha dakika 90 za mchezo baada ya kuonyesha kadi nyekundu hivyo Simba SC ilikamilisha dakika 90 ikiwa pungufu.

Meneja Mkuu, Dimitar Pantev kwenye kikosi cha leo alianza na mshambuliaji mmoja Seleman Mwalimu huku kiungo Jean Ahoua akikosa nafasi mwanzoni kabisa kwa jaribio lake kwenda nje ya lango.

Kipa Yakoub Suleman licha ya kufungwa mabao mawili aliokoa penati moja dakika ya 62 kwenye mchezo.

Simba SC haijawa na mwendo mzuri katika mechi za kimataifa msimu wa 2025/26 kutokana na kushindwa kupata ushindi hatua ya makundi.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.