Ureno Yaonesha Ubabe, Yaifumua Tanzania 10–0 Futsal Women’s World Cup

Pasig, Ufilipino — Timu ya Taifa ya wanawake ya Tanzania ya mchezo wa Futsal imeanza kwa mtihani mgumu kwenye fainali za Kombe la Dunia (Futsal Women’s World Cup 2025) baada ya kupokea kipigo kikubwa cha 10–0 kutoka kwa mabingwa wa Ulaya, Ureno, mchezo uliochezwa katika Uwanja wa PhilSports Arena jijini Pasig.

Tanzania, inayoshiriki michuano hii kwa mara ya kwanza katika historia, ilionekana kupambana lakini kiwango cha juu cha Wareno kilitawala mchezo kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho.

Magoli ya Ureno

⚽⚽ Pereira — 4’, 32’

⚽ Azevedo — 6’

⚽ Kaka — 7’

⚽ Matos — 12’

⚽ Fifo — 14’

⚽ Kika — 16’

⚽ Issa (og) — 21’

⚽ Leninha — 21’

⚽ Moreira — 24’

Matokeo hayo yameweka wazi ukubwa wa changamoto iliyopo kwenye michuano hii ya kiwango cha juu, huku Tanzania ikionekana bado kujifunza kasi, mbinu na uzoefu wa mashindano ya kimataifa ya futsal.

Ratiba ya Mechi Zijazo

Tanzania ipo Kundi C na itapambana tena katika mechi mbili muhimu:

Novemba 26, 2025: Tanzania vs New Zealand

Novemba 29, 2025: Tanzania vs Japan (mchezo wa mwisho wa kundi)

Wadau wa michezo nyumbani wanatumai kuwa Taifa Stars ya wanawake Futsal itajipanga upya na kufanya marekebisho kuelekea mechi zinazofuata ili kuongeza nafasi ya kusonga mbele.