Yanga SC 4-1 KMC FC ilikuwa kazikazi

Yanga SC 4-1 KMC FC ilikuwa kazi nzito kwa wababe wawili uwanjani Novemba 9,2025 kusaka pointi tatu ambapo dakika 45 za mwanzo mzani ulikuwa kwenye usawa.

Ni Maxi Nzengeli alifungua ukura wa mabao alipopachika bao la kuongoza dakika ya 36 likawekwa usawa na mshambuliaji wa KMC FC, Daruesh Saliboko dakika ya 42.

Kipindi cha pili, kasi ya Yanga SC iliongezeka wakafunga mabao matatu ilikuwa moja kupitia kwa Pacome Zouzoua dakika ya 72.

Wakati KMC FC wakipambana kuweka usawa bao hilo, Prince Dube ambaye alitoa pasi ya bao kwa Pacome alikwenda benchi akampisha Andy Boyeli ambaye alifunga mabao mawili.

Ilikuwa dakika ya 82 kwa mkwaju wa penati na dakika ya 90+3 kwa shuti ambalo lilimshinda mlinda mlango wa KMC FC.

Rekodi zinaonyesha kuwa tangu 2018 ni mara 15, Yanga vs KMC FC wamekutana uwanjani, ushindi kwa Yanga SC ni mechi 12, ushindi kwa KMC FC ni mechi 1 na sare ni 2.

Matokeo haya yanaifanya Yanga SC kuwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 10 baada ya mechi 4 huku KMC FC nafasi ya 16 pointi 3 baada ya mechi 16.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.