Simba SC vs TRA United mtihani mwingine kwa Pantev

MENEJA Mkuu wa Simba SC, Dimitar Pantev kwenye mtihani mwingine wa Ligi Kuu Tanzania Bara ugenini msimu wa 2025/26.

Simba SC vs TRA United unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa  Pantev kukaa benchi kwenye mechi za ligi mara baada ya kuchukua mikoba ya Fadlu Davids.

Mechi mbili ameongoza Pantev akiwa ndani ya Simba SC ilikuwa kwenye anga la kimataifa katika kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba SC imepenya hatua hiyo kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-0 Nsingizini Hotspurs ya Eswatini na mabao yote walishinda katika mchezo wa ugenini.

Pantev ameweka wazi kuwa mpango mkubwa ni kuona wanapata matokeo kwenye mechi zinazofuata ikiwa ni kwenye ligi na anga la kimataifa.

Oktoba 30,2025 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwa wababe hao wawili kuwa uwanjani kusaka pointi tatu muhimu.

Oktoba 28,2025 msafara wa kikosi cha Simba SC mapema ulianza safari kutoka Dar kuelekea Tabora kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo huo utakaorushwa mubashara na Azam TV.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.